March 27, 2016

 

Afisa wa idara ya afya nchini Pakistan aliyekuwa akisimamia kampeini ya kutoa chanjo ya kupambana na maradhi ya polio maeneoya vijijini karibu na mpaka na Afghanistan ameuawa kwa kupigwa risasi.
Bwana Akhtar Khan alikuwa katika zahanati yake ya afya wakati aliposhambuliwa na mtu aliyekuwa amejihami kwa bunduki.


Baadhi na wanamgambo na wapiganaji katika maeneo hayo wanadai kuwa dawa hiyo ya chanjo inauiwa kuwafanya watoto kutoka jamii hiyo wasiwe na uwezo wa kuzaa watakapokuwa wametimiza umri.
Kutokana na vitendo kama hivyo imekuwa vigumu kutokomeza maradhi ya polio katika mataifa hayo mawili ya Pakistan na Afghanistan .

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE