April 17, 2016


Taarifa tulizozipata kutoka mkoani Iringa zinasema mwanamuziki toka katika kundi la Tip Top Connection Tunda Man amepata ajali mapema asubuhi ya leo na dereva wa gari hilo amefariki hapo hapo.

Tunda man ameelezea tukio hilo 

                                  
 ‘Tulikua tunatoka Njombe baada ya kumaliza show yetu na tukasema bora tusilale tuwahi kufika Dar,tumetoka Njombe saa 10 alfajiri mimi nikawa nasikia usingizi nikamwambia mwanangu hebu tuendeshe kidogo,kufika kijiji cha Idetelo kilomita kama 20 au 30 kabla ya kufika Mafinga tukiwa tumelala tukashtuka Gari inaingia porini tukasikia mshindo mkubwa gari imepiga puuuh Dereva hapo hapo akawa amefariki‘
Tunda Man anamalizia kwa kusema ‘Tulikua watu watano kwenye gari aliyekaa mbele na Dereva amevunjika mkono na nyama zimechanika,kuna mtu aliyekua nyuma mapafu yamepasuka,Mimi nipo poa,kwa sasa hivi tuko Mafinga hapa Hospitali ya Wilaya tunaangalia taratibu za kuchukua mwili tuupeleke Kilosa kwa ndugu zake,marehemu aliyefariki anaitwa Mussa lakini watu wengi wanamjua kwa jina la Man katuzo.



Babu Tale naye anathibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

  • babutaleNimepokea simu nyingi za kuulizwa hali ya msanii wangu @tundamantz mungu mkubwa ametoka salama ingawa wamepata mtihani mkubwa wa kumpoteza dereva aliyekua anaendesha gari yao amefariki Hapo Hapo. Kazi yake mola aina makosa 



    Tunda





3flkp 

4flkp 

5flkp 

6flkp 

7flkp 

12flkp 

11flkp 

10flkp 

9flkp 

8flkp

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE