Waziri wa Habri, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye ambaye kwa sasa yupo ziarani katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ameahidi kuwa atamaliza vitendo vya rushwa michezoni baada ya kuonekana kushamiri kwa vitendo hivyo hadi kupelekea baadhi ya vilabu kufungiwa.
Mo Blog imekuandalia habari picha jinsi Waziri Nape alivyosema akiwa mkoani Tabora.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na Watumishi wa Serikali pamoja na Wadau walio chini ya wizara yake wa mkoa wa Tabora ambapo aliwaambia kuwa atawaondoa wala rushwa na matapeli katika michezo nchini.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na watumishi wa serikali waliochini ya wizara yake pamoja na washika dau wa habari, utamaduni sanaa na michezo wa mkoa wa Tabora ikiwa sehemu ya ziara yake yenye lengo la kuifanya wizara yake kumfikia kila mtu nchini na si kuishia Dar es Salaam tu.
 Katibu wa CHANETA mkoa wa Tabora Mwalimu Mwajuwa Yusufu akisoma taarifa ya chama chao pamoja na changamoto zinazowakabili kwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye.
Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu mkoa wa Tabora, Ndugu Lawrence Safari akichangia maoni mbali mbali ya kuboresha michezo nchini kwenye mkutano na Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye.
 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi za CCM mkoa wa Tabora ambapo aliwataka Mawaziri wanaofanya ziara kwenye mikoa mbali mbali wajenge utamaduni wa kupitia kwenye ofisi za chama na kusaini kitabu cha wageni kwani chama ndicho kimetengeneza ilani inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM akizungumza na viongozi wa CCM mkoa wa Tabora mara baada ya kumaliza kutia saini kitabu cha wageni na kuwataka wana CCM wote kuisoma kwa umakini ilani ya uchaguzi ya CCM 2015-2020 kwani ndio inayotekelezwa na serikali ya awamu ya 5.
 Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akipata maelezo ya mitambo ya kurusha matangazo ya TBC mkoani Tabora kuroka kwa Mkuu wa kituo cha TBC Tabora Ndugu AMani Ganally Kalelesi.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye (mwenye kaunda suti nyeusi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wasanii wa kwaya kutoka kikosi cha 823 KJ Msange JKT  mkoani Tabora.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza na watumishi na wadau walio chini ya wizara yake wa mkoa wa Singida ambapo alisisitiza kuwa kila manispaa inatakiwa kuwa na afisa habari ambaye anapata nafasi ya kuingia kwenye vikao vya maamuzi.