Amesema
uamuzi huo ni mkakati wa kuliwezesha shirika hilo kuweza kujiendesha
kwani awali lilikuwa likitumia fedha nyingi kwa urushaji wa matangazo ya
bunge bila ya malipo.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, amesema hayo
jijini Mbeya, wakati akizungumza na wadau wa habari, michezo, utamaduni
na watendaji wa serikali mikoa ya Mbeya na Songwe,
Amesema
shirika la utangazaji la Taifa, TBC, lilikuwa linaagizwa kurusha
matangazo ya Bunge bila ya malipo ambapo kwa mwaka shirika lilikuwa
likitumia bilioni 4 kwa mapato yake ya ndani na kulifanya kushindwa
kukarabati mitambo pamoja na mslahi ya watumishi hivyo, uamuzi huo
ulikuwa sahihi licha ya wananchi wengi kuonesha kutoridhishwa no.
Amesisitiza
kuwa suala hilo litaleta heshima ya Bunge kwani ilifika wakati, baadhi
ya wabunge walikuwa wakitoa lugha za maudhi pamoja na kucheza sarakasi
mambo ambayo yalikuwa yakivunja heshima ya bunge.
Amesema
kutokana na hatua hiyo Bunge lenyewe ndio limechukua dhamana ya
kuanzisha studio yake hivyo kutoa fursa kwa televisheni nyingine kurusha
matangazo ya moja kwa moja lakini kulingana na vigezo na masharti
yatakayohalalishwa na mamlaka hiyo.
Akizungumzia
sheria ya baraza la michezo ambayo imekuwa ikilitaja suala la michezo
ni hiari, Nape amesema kwa sasa serikali ipo katika mchakato wa
kuirasimisha sheria hiyo ili iendane na sera ya michezo ambayo imeweka
wazi kwamba michezo kuwa shughuli rasmi ya kiuchumi, ambapo katika kikao
hicho wajumbe walipata nafasi ya kuwasilisha kero na changamoto
mbalimbali wanazokumbana nazo.
Aidha,
akijibu risala iliyotolewa na Chama cha waandishi wa habari Mkoa wa
Mbeya, ambayo ilimuomba kiongozi huyo kuhakikisha anausimamia mswada huo
wa habari katika kulinda maslahi ya wafanyakazi,Nape, aliwataka
waandishi wa habari kutambua kuwa maslahi yao wanayoyapigania kutoka kwa
waajiri wao, yanajibiwa kwenye mswaada wa sheria ya huduma wa vyombo
vya habari.
Alisema,
wakati ule ulikuwa ni mwishoni mwa Bunge lililopita hivyo kwa sheria na
kanuni za Bunge mswaada huo unatakiwa ukasomwe tena kwa mara ya kwanza,
kwa hiyo umefikia pahala pazuri, na kuhakikisha kwamba maslahi ya
waandishi wa habari mule ndani yamelindwa.
Pia,
Waziri huyo, aliongeza kuwa serikali inaangalia utaratibu wa kuvifuta
baadhi ya vyuo vinavyotoa elimu ya habari ambavyo havina sifa, kwani
vimekuwa vikitoa waandishi wa habari amaboa hawana sifa na kazi yao
imekuwa ni kuupotosha umma.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment