April 05, 2016

 
Macho na maskio ya watanzania, kuhusu Serikali ya umoja wa kitaifa Zanziba, chanma gani kitatoa makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Zanziba? Katika serfikali iliyopita, iliyoundwa na vyama viwili vya Siasa vya Zanzibar, Makamu wa kwanza wa Rais alikuwa Maalim Seif Sharif Hamad kutoka Chama Cha Wananchi CUF.

   Sasa kutokana na chama cha CUF kutoshiriki katika uchaguzi uliopita, vyama vilivyoshiriki havikukidhi vigezo.

 Soma tamko la Rais wa Zanzibar hapa:
Akihutubia katika uzinduzi wa Baraza la 9 la Wawakilishi Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein amesema kuwa kwenye uchaguzi wa Marudio uliofanyika Machi 20, hakuna chama kilichopata kura za rais kwa zaidi ya asilimia 10 isipokuwa CCM. Pia amesema kuwa hakuna chama kilichopata wabunge wengi isipokuwa CCM.Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, hakuna chama kilichopewaa ridhaa ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa isipokuwa CCM.
Kwamba, Makamu wa Pili amechaguliwa kwa mujibu wa sheria na hakuna nafasi Kikatiba ya kuteua Makamu wa Kwanza wa Rais ama Mawaziri kutoka Upinzani. Amesema hayo ni maamuzi ya wananchi na ni lazima yaheshimiwe. Wananchi Wamewakataa wapinzani na kuiamini CCM.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE