Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli, kesho
Jumatano, Aprili 06 mwaka huu anatarajia kufanya ziara wilayani Ngara
mkoani Kagera, kwa ajili ya kuzindua daraja la Rusumo linalounganisha
nchi ya Tanzania na Rwanda pamoja na jengo la Kituo cha Pamoja cha
Forodha - (OSBP).
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya Habara, Mkuu wa wilaya ya Ngara Bi
Honoratha Chitandaa amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumpokea
Rais Magufuli na kuongeza kuwa halmashauri ya wilaya hiyo imejipanga
kuwasafirisha wananchi watakaokosa usafiri ili kufanikisha mapokezi.
Bi
Chitanda amesema pia kamati ya ulinzi na usalama imejipanga kuhakikisha
ziara ya Rais inakwenda vizuri bila kuingiliwa na dosari yoyote
inayoweza kupelekea uvunjifu wa amani na kuwataka wananchi wote kutii
sheria.
Katika
ziara hiyo Rais magufuli anatarajia kukutana na Rais wa Rwanda, Paul
Kagame atakayeshirikiana naye katika Uzinduzi wa Daraja la Rusumo
linalounganisha nchi mbili za Tanzania na Rwanda.
Baadaye, marais hao wataelekea Kigali-Rwanda ambapo watafanya mazungumzo ya pamoja.
Rais Magufuli pia ataweka shada la maua katika makumbusho ya mauaji ya kimbari ya Rwanda 1994 mjini humo.
Rais Magufuli pia ataweka shada la maua katika makumbusho ya mauaji ya kimbari ya Rwanda 1994 mjini humo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment