April 05, 2016


Gadna 2
Gardner akisaini mkataba wake mpya pembeni ya mkuu wa vipindi CloudsFM Shaffih Dauda


Historia huwekwa na kuvunjwa na pengine anaye iweka ndio anaweza kuivunja na kama sio yeye basi mtu mwingine anaweza kuivunja, Kwa tasnia ya Burudani na Habari Tanzania ina jina ambalo kamwe haliwezi kusahaulika kwanamna yoyote ile naamini ukilijua jina hili huwezi kuacha kukubaliana na mimi.


Anaitwa Gadner G Habash Maarufu kama Captain alipokuwa anaaga Clouds Fm miaka kadhaa iliyopita alisema kwamba “Napumzika kutangaza lakini nitarudi”.


Maneno haya yalitimia miaka kadhaa iliyopita aliporudi kwenye fani rasmi baada ya kukaa nje kwa muda mrefu alianzia kituo cha redio cha Times Fm akasikika na kipindi chake kilichokwenda kwa jina la “Masikani” kilichokuwa kinaanza saa 10 jioni hadi Saa1 usiku, alidumu pale lakini baadae alihamia kituo cha redio cha E-FM nakuanzisha kipindi cha “UBAONI” ambacho kilikuwa kiaruka sa 9 mchana hadi sa 1 usiku.


Lakini usemi wake wa kwamba nitarudi hatimaye umetimia na Rasmi kupitia kipindi cha XXL na Jahazi ambapo ametambulishwa rasmi kuwa amerudi Clouds Fm maarufu kama Radio ya watu na ataungana na timu ya kipindi cha Jahazi  ya Kibonde, George Bantu, Hamisi Dakota na Emanuel Likuda kinachoruka kuanzia sa 10 jioni hadi saa 1 usiku.


Ikumbukwe tu kuwa Gadner ndio mwanzilishi wa kipindi hicho na ameahidi mambo mengi mapya kwenye msimu mpya unaoanza tarehe April 11.


Unaweza kuisikiliza hapo chini mizinga 12 aliyopigiwa Gadner baada ya kurejea Clouds Fm.


0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE