April 05, 2016



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bibi Angela Kairuki amewapa wiki moja waajiri wa sekta za umma nchini kukamilisha na kuwasilisha taarifa kuhusu watumishi hewa.

Bibi Kairuki ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam alipokua akiongea na waandishi wa habari kuhusu taarifa za awali juu ya watumishi hewa zilizowasilishwa na Wakuu wa Mikoa nchini.


Amesema kuwa taarifa za Machi 1 hadi April 4 mwaka huu zinaonyesha watumishi 4,317 waliondolewa katika Payroll ya Serikali ikiwa ni kasi ya kuondoa watumishi ambao utumishi wao umekoma kwa kipindi kifupi ambapo haijawahi kufikiwa kwa kipindi cha nyuma ikiwa ni mwitikio wa agizo la Rais Dkt Magufuli.


"Kutokana na Mfumo wa HCMIS ambao hufungwa kila tarehe 5 ya kila mwezi umewezesha Watumishi wa Serikali 1,284 kufutwa kwa Aprili 1 hadi 4 ikiwa imejumuishwa watumishi hewa, waliostaafu, walioacha kazi waliofukuzwa na waliofariki dunia"Amesema Angela.


Angela amesema kuwa muda wa kufunga Payroll umeongezwa na utafungwa Aprili 12 ili kuhakiki watumishi wote wa serikali ambao hawastahili kuwepo kwenye Payroll"


Pia amesema kuwa baada ya tarehe hiyo Ofisi yake itafanya ukaguzi kwenye taasisi na mamlaka mbalimbali za Serikali ili kuhakikisha wale ambao hawawajibiki au kutimiza wajibu wao katika eneo la usimamizi wa rasilimali watu wanachukuliwa hatua stahiki kwa mujibu wa sheria.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE