Baada ya baadhi ya Wabunge wa vyama vya
upinzani Tanzania kumtaka Rais Magufuli kuanika hadharani mshahara wake
pamoja na makato ya kodi, President Magufuli ambaye ni Rais wa awamu ya
tano kwenye Jamuhuri ya muungano wa Tanzania amekubali kuutaja mshahara
wake.
Kama kawaida yake yeye ni shabiki wa
kipindi cha TV cha Clouds 360 on CloudsTV ambacho alikipigia simu kwa
suprise March 17 2016, sasa wakati anatazama kipindi hicho April 1 2016
akiwa nyumbani kwao Chato, Rais Magufuli akaona Watangazaji wakisoma
magazeti na kukawa kuna habari moja kwamba Wabunge Zitto Kabwe na Tundu
Lissu wanamtaka ataje kiwango cha mshahara anaolipwa kama rais wa
Tanzania.
Muda mfupi baadae President aliwasiliana na Watangazaji wa Clouds360 na kusema mshahara wake ni shilingi za kitanzania MILIONI 9.5 na akasema yuko tayari kuonyesha nyaraka za malipo ya mshahara wake na kutoa mchanganuo akimaliza mapumziko Mkoani Geita.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment