MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametangaza neema kwa waendesha bodaboda katika jiji la Dar es Salaam kwa kuwadhamini pikipiki kutoka kwa kampuni zinazofanya biashara hiyo.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana waendesha bodaboda kwa ajili ya kuboresha kazi hiyo katika kuwaletea maendeleo ya uchumi, amesema kuwa udhamini wa pikipiki kwa atakayekopeshwa kulipa sh.25,000 kila wiki na baadae kumiliki pikipiki hizo.
Makonda amesema umefika wakati wa vijana kumiliki pikipiki zao na sio
kufanya biashara hiyo za watu ambao wanachukua fedha nyingi na wao
kuendelea kuwa na maisha magumu.
Source: Cloudsfm Radio
Source: Cloudsfm Radio
0 MAONI YAKO:
Post a Comment