April 19, 2016

Idadi ya wafanyakazi hewa katika mkoa wa Shinyanga ambao awali ulidaiwa kutokuwa na wafanyakazi hao kabisa, imeongezeka na kufikia 226.

Hayo yamebainishwa leo na Rais John Magufuli katika uzinduzi wa Daraja la Kigamboni, ambapo alisisitiza kuwa serikali yake haitawafumbia macho viongozi ambao kwa namna moja au nyingine wataruhusu mianya ya ubadhirifu wa fedha katika maeneo yao.

”Mkoa wa Shinyanga kwa taarifa nilizonazo hadi sasa wameshapatikana wafanyakazi hewa 226 kutoka ‘zero’ hivyo ni lazima tuwajibike kwa watanzania wanyonge,” amesema Rais Magufuli.

Wakati wa kuwasilisha ripoti ya Mikoa Serikalini aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela alisema mkoa wake hauna mtumishi hewa hata mmoja jambo lililopelekea Rais Magufuli kuunda tume iliyobaini watumishi  hewa  45 katika awamu ya kwanza.

Baada ya kubainika uwepo wa watumishi hao, Raisi alitangaza kutengua uteuzi wa Mkuu huyo wa Mkoa kwa kutokuwa makini na taarifa anazopewa na wasaidizi wake.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE