Mwanamuziki Chris
Brown amesema kuwa alitaka kujiua baada ya kumshambulia aliyekuwa
mpenziwe Rihanna kabla ya tuzo za Grammy mwaka 2009.
Katika
kipande kifupi cha makala yake ya 'Karibu katika maisha
yangu',mwanamuziki huyo wa mtindo wa R & B amesema kuwa uhusiano wao
ulikuwa kama ndoto lakini akajihisi kama hayawani.''Nilikuwa katika kilele cha dunia,nyimbo zangu zikiongoza,nikapendwa na wengi nchini Marekani kabla ya kuanguka hadi kuwa adui wa uma'',alisema.
Kifungo hicho kilisitishwa mwaka jana baada ya jaji moja kusema kuwa nyota huyo amekamilisha mahitaji yake yote na kufunga kesi hiyo rasmi.
''Nilikuwa nikilala.Sikuweza kula,nilijihisi maarufu'',alikiri.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment