Bongo Star Search ni shindano pekee kwa Tanzania la kusaka vipaji kwa vijana wenye uwezo wa kuimba.
Madam
Rita kupitia kampuni yake ya Benchmark Production alikuwa na malengo
mazuri ya kuanzisha shindano hili ambalo watanzania tulikuwa tunaangalia
mashindano kama haya katika nchi za nje tu.
Kwa
mara ya kwanza shindano la BSS lilianza mwaka 2007 na lilizalisha
vipaji kama, Kala Jeremiah, Baby Madaha, na aliyekuwa mshindi wa
shindano hilo Jumanne Iddi ambaye kwa sasa amepotea kwenye ramani ya
muziki.
Mashindano
ya BSS, msimu wa nane mwaka 2015 yamesaidia kuvitambua vipaji vingi
vilivyokuwa vimejificha. Washiriki watano waliofanikiwa kuingia kwenye
fainali za shindano hilo ni Kayumba Juma, Nassibu Fonabo, Frida Amani,
Angel Mary Kato na Kelvin Gason.
Tunakumbuka
kuwa kwenye shindano hilo, Kayumba Juma alifanikiwa kushinda na
kufanikiwa kupata mkwanja wa shilingi milioni 50. Moja ya ahadi
zilizotoka kwenye mashindano hayo ni kuwa top five yote itakuwa chini ya
menejimenti ta Tip Top Connection.
Ni
miezi mingi imepita mpaka leo tangu shindano hilo lifanyike, mpaka sasa
ni wimbo pekee wa Kayumba Juma ‘Katoto’ ndiyo umeweza kutambulishwa kwa
mashabiki wa muziki, je wako wapi hao wasanii wengine walioingia kwenye
ile top five?
Tunajua
kuwa mkataba na washiriki haona kuwa chini ya menejimenti ya Tip Top
Connection ilikuwa ni ya mwaka mmoja tu, mpaka sasa ni miezi mingi
imeshapita bado hatujaona chochote kipya na miezi michache tu imebakia
mkataba huo uweze kuisha.
Je
ndani ya hiyo menejimenti itaweza kusaidia hao vijana kuachia kila
mmoja nyimbo mbili ndani ya hii miezi iliyobakia? Sina uhakika na hilo
kama litawezeka.
Siku
chache zilizopita Babu Tale aliongea kwenye kipindi cha The Chart Show,
kinachoruka kupitia Times FM alisema kuwa muda siyo mrefu kuna msanii
mmoja kati ya wale wasanii ataachia wimbo wake. Sina shaka kwa lile
alilolisema Babu Tale, wasi wasi wangu unabaki kuwa menejimenti ya Tip
Top Connection inasimamia wasanii wengi kwa sasa na kila msanii
anahitaji msaada kutoka kwenye menejimenti hiyo.
Je hawa wasanii wa BSS wamewekwa kwenye chumba gani kwa sasa ndani ya nyumba ya menejimenti hiyo?
By Explicity
0 MAONI YAKO:
Post a Comment