April 17, 2016


Mahakama kuu ya Mombasa imemhukumu Kifo mwanamume aliyekutwa na hatia ya kumuua  kiongozi wa dini Sheikh Mohammed Idris.
Mohamed Soud amekutwa na hatia ya kumuua Sheikh Idris aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la wahubiri  CIPK.
Uamuzi huo umetolewa na jaji wa mahakama kuu ya Mombasa Martin Muya .
Jaji Muya amesema ushahidi ulionesha kuwa mshukiwa alipatikana nyumbani kwake na bunduki, Guruneti na unga unaoaminika ulinuiwa kutengeneza vilipuzi.
 Amesema ushahidi uliotolewa ni wa kuaminika kwa kuwa mshukiwa alikamatwa na maafisa wa Flying Squad ambao hawajawahi kuwa na uhusiano wa karibu na mshukiwa.
Kabla ya uamuzi kutolewa, wakili wa mlalamishi Chacha Mwita aliiomba mahakama imhukumu kifungo cha maisha cha nje ya jela.
Lakini Jaji Muya akasisitiza kuwa hakuna adhabu nyingine ya kosa la mauaji kando na hukumu ya Kifo.
Sheikh Mohamed Idris aliuawa tarehe 10 mwezi Juni mwaka 2014 kwa kupigwa risasi nje ya msikiti karibu na nyumbani kwake eneo la Likoni kabla ya mshukiwa Mohamed Soud kukamatwa siku tatu baadaye katika barabara ya kutoka Likoni kuelekea Ukunda .

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE