April 17, 2016

Capture


MATUMIZI ya simu za kisasa (smartphone) yamezua maneno na uvumi wa kila aina katika blogu, magazeti mbalimbali, barua-pepe, mitandao ya WhatsApp na Facebook, hata hivyo, mtumizi wa simu hizi hatakiwi kuamini kila kitu anachokiona kwenye mitandao ya Intaneti au mahali popote. Siri, au mambo muhimu kuhusiana na simu za aina hiyo ni hizi zifuatazo

Siri ya 1: Mifumo ya kisasa ya mawasiliano na ya kuongoza ndege ni yenye utaalamu wa hali ya juu. Hivyo, hata kama ndege itakuwa ina watu wengi walio na imejaa simu za mkononi kiasi gani simu hizo haziwezi kuathiri mifumo hiyo ya mawasiliano katika ndege hiyo.
Capture 0 
Siri ya 2: Petroli hulipuka au husika moto kirahisi hata kwa cheche tu. Cheche inaweza ikatoka katika viberiti, vidude vya kuwashia sigara au hata umeme, lakini si kutoka katika simu ya mkononi. Wasiwasi uliopo kwamba simu mbovu au hata betri yake inaweza kutoa cheche au moto ni jambo ambalo haliwezekani na hapana tukio lolote lililothibitishwa kutokana na dhana hiyo.

Siri 3: Vyombo vyote vya elektroniki ambavyo vina betri ambazo baada ya muda hulazimika kuchajiwa, vina mifumo ya ndani kwa ndani ya usalama inayozuia nguvu ya umeme kuzidi na hivyo kuleta madhara. Mara tu betri inayochajiwa ikifikia kiwango chake kinachotakiwa, simu hiyo itaacha yenyewe kupokea umeme, licha ya kwamba mashine ya kuchajia inaweza, katika matukio kadhaa, ikaendelea kupokea umeme kidogo.

Siri ya 4: Chombo chochote kinachotumia betri kama vile simu ya mkononi au kompyuta-mpakatol, uwezo wa betri yake unahusiana na muundo au utendaji kazi wa mashine husika. Hivyo, ukiwa na simu mbili zinazofanana za mkononi, ile ambayo inakaa zaidi kwenye chaja ni ile ambayo ina kiwambo na vikorombwezo vingi zaidi vya kielektroniki.
Capture\
Siri ya 5: Mifumo mingi ya kufungulia kurasa kwenye simu (browsers) inatumika kutunza kumbukumbu ya mtumiaji wakati anatumia.

Siri ya 6: Ni kweli kumekuwepo matukio machache ya simu za mkononi kulipuka, lakini ukweli ni kwamba ni betri ndizo husababisha moto na kulipuka, na si simu zenyewe.

Siri ya 7: Simu yoyote bora kutoka katika kampuni yoyote maarufu lazima ifanyiwe jaribio la kuhakikisha kwamba simu hiyo haitatoa mionzi mingi kiasi cha kuweza kusababisha madhara. Jaribio hilo huitwa Specific Absorption Rating – SAR.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE