
Mke wa Ndanda Kosovo ‘Kichaa’, aitwaye, Loving Chitoto.
Mkewe wa muimbaji wa muziki wa dansi nchini aliyezikwa jana marehemu Ndanda Kosovo aitwaye Loving Chitoto, amesimulia mazito juu ya
mumewe.
Akizungumza
na paparazi wetu nyumbani kwake Kionondoni-Hananasif, Chitoto
alikumbusha kuwa alikutana na Ndanda mwaka 1999, kabla ya mwaka 2000
kumuimba katika wimbo wake wa Prison maarufu kama Wajelajela na kabla ya
kutimkia Stono Musica.
Akielezea
mapenzi yao, Chitoto alisema kama Mungu angewajaalia basi wangekuwa na
watoto wanne hivi sasa, lakini wamebakia na mtoto mmoja aitwae Okito
ambaye Septemba, mwaka huu anatarajia kutimiza miaka mitatu.

Ndanda Kosovo enzi za uhai wake.
Akifafanua, Chitoto alisema awali mwanzoni mwa mapenzi yao, walibahatika kupata mtoto aliyeitwa Patrick lakini alifariki dunia.
Baada
ya hapo alipata ujauzito mwingine na kufanikiwa kupata watoto mapacha,
lakini nao walifariki dunia muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Aliendelea
kusema licha ya mikasa hiyo hawakukata tamaa, waliendelea na mapenzi
yao mpaka alipopata ujauzito na kumpata Okito ambaye Mungu amempa uzima
hadi sasa.
“Ukweli
siwezi kumsahau baba watoto wangu Ndanda, tumetoka mbali na tulitarajia
kufika mbali zaidi, lakini kazi ya Mungu haiingiliwi,” alisema Chitoto
huku akijifuta machozi.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya mwanamuziki huyo, King
Dodoo marehemu anatarajiwa kuzikwa leo Jumatano kwenye Makaburi ya
Kinondoni jijini Dar ambapo maandalizi yamefanyika kwenye nyumba ya
Ubalozi wa Congo DRC iliyopo Kinondoni-Hananasif jijini.
Dodoo
alisema wameamua kumzika marehemu hapa nchini kufuatia wosia wake
alioutoa mbele ya Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo,
Nape Nnauye wakati akizungumza na wanamuziki wa dansi katika Ukumbi wa
Vijana Kinondoni mwezi uliopita.
Katika
kikao hicho Ndanda alisimama na kusema endapo akifa basi maiti yake
izikwe hapa Tanzania kwa kuwa ndipo mahali alipopatia mafanikio makubwa
ya kimuziki na anahisi ndiyo sehemu ambayo atazikwa na watu wengi kuliko
Lubumbashi alikozaliwa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment