Kwa mujibu wa Mbunge wa Jimbo la Mikumi ambaye pia ni rapa, Joseph
‘Prof: Jay’ Haule, amedai alipigiwa simu na mkuu wa wilaya ambayo Mikumi
inapatikani kujulishwa kuwa alitumiwa barua kuomba achangie mchango wa
shilingi milioni 5 kwa ajili ya mbio za Mwenge.
Akizungumza na wananchi wa Ruaha Mkoani Morogoro, Prof Jay amesema
alimjibu mkuu wa Wilaya hiyo kuwa, kuliko kuchangia Mbio za Mwenge ni
bora fedha zake aelekeze kwenye maendeleo ya Wananchi.
“Wakati nakuja njiani Mkuu wa Wilaya alinipigia simu, akanambia Mh
tumeleta barua ofisini kwako kuomba mchango wako katika mbio za mwenge,
nikamwambia daah hizo hela za kuchangia karibu milioni tano, ni bora
nipeleke Ruaha maji yatoke tu” Alisema.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment