April 13, 2016


 
 
 Sanduku lenye Mwili wa Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo ukiwasili mapema leo mchana katika  nyumba ya Ubalozi wa Congo,iliopo Hananasifu-Kinondoni jijini Dar,kwa ajili ya kuagwa na hatimae mazishi yake kufanyika jioni ya leo katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar.

 Waziri Nape Nnauye akisalimiana na Waombolezaji waliofika kwenye msiba wa Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini, Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo ambaye  anatarajiwa kuzikwa jioni ya leo Makaburi ya  Kinondoni jijini Dar.

 
  Waziri wa Habari,utamaduni,Sanaa na Michezo.Mh Nape Nnauye akisalimiana na Waombolezaji waliofika kwenye msiba wa Mwanamuziki Mkongwe hapa nchini,Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo ambaye  anatarajiwa kuzikwa jioni ya leo Makaburi ya Kinondoni jijini Dar. 
 
  Waziri wa Habari,utamaduni,Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akitoa salamu za rambirambi kwa Waombolezaji, wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo,katika nyumba ya Ubalozi wa Congo,iliopo Hananasifu-Kinondoni jijini Dar ,Ndanda Kosovo anatarajiwa kuzikwa jioni ya leo Makaburi ya Kinondoni jijini Dar. 
 
  Baadhi ya Marafiki ndugu jamaa na wanamuziki wenzake wakiwa wamekusanyika nje ya nyumba ya Ubalozi wa Congo,iliopo Hananasifu-Kinondoni jijini Dar ,wakisubiri kuwasili kwa mwili wa Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo kwa ajili ya kuagwa na hatimae mazishi yake kufanyika leo alasiri katika makaburi ya Kinondoni.
  Mwanamuziki Lady Jay Dee akiwasili kwenye kuaga mwili wa Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo mapema leo mchana.
 Sanduku lenye mwili wa Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo likiwa mbele ya Waombolezaji tayari kwa kuanza kumuaga.
 Baadhi ya Marafiki,Ndugu na Jamaa wakiwemo Wanamuziki wenzake wakiwa wamejipanga nje ya nyumba ya Ubalozi wa Congo,iliopo Hananasifu-Kinondoni jijini Dar, wakisubiri kuupokea mwili wa Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo kwa ajili ya kuagwa na hatimae mazishi yake kufanyika leo alasiri katika makaburi ya Kinondoni,jijini Dar.
 
  Waombolezaji wakiwa katika hali ya huzuni. 
 
 Baadhi ya Marafiki ndugu jamaa na wanamuziki wenzake wakiwa wamekusanyika nje ya nyumba ya Ubalozi wa Congo, iliopo Hananasifu-Kinondoni jijini Dar, wakisubiri kuwasili kwa mwili wa Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo kwa ajili ya kuagwa na hatimae mazishi yake kufanyika leo alasiri katika makaburi ya Kinondoni.
 
 Mama wa Marehemu Onawembo Ngongo a.k.a Ndanda Kosovo akilia kwa uchungu mara baada ya kuwasili mwili wa Marehemu mwanae kwenye nyumba ya ubalozi wa Congo,Hananasifu-Kinondoni jijini Dar mchana huu.
 
 
  Baadhi ya waombolezaji wakilia kwa uchungu. 
 
 Baadhi ya Wanamuziki na Ndugu Jamaa na marafiki wakiwa kwenye msiba huo.
 
 Shughuli ya mazishi ya staa wa Muziki aliyefariki mwishoni mwa wiki iliyopita, Ndanda Kosovo ‘Kichaa’ katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar, Mwanamuziki huyo Ndanda Kosovo ‘Kichaa’ amezikwa leo Jumatano kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar ambapo maandalizi yamefanyika kwenye nyumba ya Ubalozi wa Congo DRC iliyopo Kinondoni-Hananasif jijini.
Dodoo alisema wameamua kumzika marehemu hapa nchini kufuatia wosia wake alioutoa mbele ya Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye wakati akizungumza na wanamuziki wa dansi katika Ukumbi wa Vijana Kinondoni mwezi uliopita.
Katika kikao hicho Ndanda alisimama na kusema endapo akifa basi maiti yake izikwe hapa Tanzania kwa kuwa ndipo mahali alipopatia mafanikio makubwa ya kimuziki na anahisi ndiyo sehemu ambayo atazikwa na watu wengi kuliko Lubumbashi alikozaliwa.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE