Mfalme wa muziki wa taarab Mzee Yussuf amesema zamani kabla hajaanza kuimba muziki wa taarab alikuwa akifanya muziki wa Hip Hop.
Akizungumza
na Bongo5 Jumatano hii, Mzee Yussuf amesema ukifika wakati atatoa kibao
kimoja cha muziki wa Hip Hop ili kuwaburudisha mashabiki wake.
“Mimi
zamani nilikuwa chini ya Ruge, nilikuwa nachana kabisa, lakini sio ile
ngumu, yangu ilikuwa ina ‘ubongofleva’,” alisema Mzee Yussuf. Lakini
baada ya kukaa muda mrefu ndio nikaanza kuimba taarab lakini ipo siku
nitawafurahisha mashabiki wangu kwa wimbo mmoja,”
Katika hatua nyingine Mzee Yussuf amewataka mashabiki wa muziki wa taarab kukaa mkao wa kula kwa ajili ya kazi zake mpya mbili
0 MAONI YAKO:
Post a Comment