Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Kenya, Mheshimiwa Raila Amoro Odinga amemtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyopo mapumzikoni katika Kijiji cha Kilimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita.
Mheshimiwa Odinga ambaye ameongozana na mkewe Mama Ida Odinga na Binti yake Winnie Raila Odinga, wametua kwa Helkopta katika uwanja wa Shule ya sekondari ya Chato leo tarehe 02 April, 2016 majira ya saa 11 jioni na baadaye kuelekea nyumbani kwa Rais Magufuli ambako wamepokelewa na wenyeji wao Rais Magufuli
mwenyewe na Mkewe Mama Janeth Magufuli.
Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga akisalimiana na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli mara baada ya kuwasili Chato
Waziri
Mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga akisalimiana na mama mzazi wa Rais
Dkt. John Pombe Magufuli, Bi Suzana Joseph Magufuli mara baada ya
kuwasili Chato Mkoani Geita.
Source: Cloudsfm Radio
0 MAONI YAKO:
Post a Comment