April 02, 2016

Spika wa bunge la serikali ya Gabon ajiuzulu 
Spika wa bunge la serikali ya Gabon Guy Nzouba Ndama ametangaza kuwasilisha barua ya kujiuzulu kufuatia uchaguzi wa rais unaokaribia kufanyika nchini humo.
Ndama aliarifu kuchukuwa uamuzi huo kutokana na mizozo ya kisiasa iliyokuwepo miongoni mwa wabunge wa chama tawala na upinzani.
Ndama alitangaza bungeni siku ya Alhamisi kuwa amewasilisha barua ya kujiuzulu kwa rais Ali Bongo Ondimba siku ya Alhamisi.
Kwa upande mwengine, viongozi wa upinzani wanaarifiwa kumpongeza Ndama kwa kuchukuwa hatua hiyo ya kujiuzulu kama spika wa bunge.
Viongozi wa chama tawala wametoa maelezo na kuarifu kwamba wamepokea ombi la Ndama na hivi karibuni watamchagua spika mwengine wa bunge.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE