KAMPUNI
ya Mawasiliano ya simu Tanzania TTCL imeiomba serikali kuwamilikisha
mkongo wa mawasiliano wa Taifa ilikampuni hiyo waweze kuuendesha wao
kutokana na uwezo walionao na mafundi na wataalamu wa kutosha.
Ombi
hilo lilitolewa na meneja wa TTCL Mkoani Kigoma,Abdalah Lugage wakati
akitoa taarifa ya Mkoa kwa Waziri wa ujenzi uchukuzi na Mawasiliano
wakati alipotembelea ofisi hizo.
Alisema
shirika hilo linauwezo wa kusambaza mawasiliano katika ofisi zote na
mpaka sasa wamefikia uwezo wa internet 4G ambayo inatumiwa na ofisi zote
za serikali na binafsi.
Lugage
alisema wao kama Shirika la mawasiliano wanauwezo wa kumiliki mtambo
huo wa taifa kutokana na uwezo mkubwa na kazi nzuri wanayo ifanya
kuwahudumia watanzania katika mawasiliano.
Waziri
wa ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano,Makame Mbarawa alisema Serikali
haiwezi kuwaachia TTCL kumiliki mkonga Wa taifa kwa asilimia zote jambo
linaloweza kupelekea Makampuni mengine kuja kununua Mkongo na kuuwa
shirika.
Mbarawa
alisema atajaribu kuongea na Serikali na Viongozi ikiwezekana serikali
imiliki 30% na shirika hilo kumiliki 70% ya Mkongo wa Taifa ilikuyafanya
makampuni mengine kutumia Mkongo wa Taifa na serikali kujiingizia
mapato kupitia Mawasiliano.
"Kuhusiana
na suala la Mkongo wa Taifa nitaongea na TCRA muweze kuingia kwenye
ubia na serikali katika umiliki wa Mkongo wa Taifa naniwatake mboreshe kwanza mikongo na mitambo yenu ilitujilidhishe na huduma zenu" alisema Mbarawa.
Mbarawa
alisema pia Serikali inampango wa kuboresha ubora wa internet kufikia
masafa ya 800 ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuifanya shirika hilo kufanya
kazi kwa uhakika zaidi.
Aidha amewaomba watumishi wote waweze kufanya kazi kwa umakini na ushirikiano ilikuweza kutoa huduma zenye ufanisi na umakini wa hali ya juuu.
Aidha amewaomba watumishi wote waweze kufanya kazi kwa umakini na ushirikiano ilikuweza kutoa huduma zenye ufanisi na umakini wa hali ya juuu.
Kwa
upande wake Afisa mtendaji mkuu wa TTCL nchini Dr Kamugisha Kazaura
alisema serikali inampango wa kuiboresha kampuni hiyo ilikuweza
kuwarahisishia Watanzania huduma za Mawasiliano,hivyo
aliwaahidi watanzania shirika hilo limejipanga ipasavyo kuhakikisha
huduma hizo zinaboreshwa na Wanatanzania wanapata huduma zenye viwango
vya kujitosheleza.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment