Shirika la Afya Duniani la WHO limethibitisha kugundulika kwa kesi mpya ya virusi vya Ebola nchini Liberia.
WHO ilitoa maelezo na kubainisha kufariki kwa mwanamke mmoja mwenye umri wa 30 siku ya Alhamisi mchana kutokana na virusi vya Ebola katika mji mkuu wa Monrovia nchini Liberia.
Wizara ya afya ya Liberia ikishirikiana na WHO imetuma timu ya maafisa wa afya katika eneo alilokuwa akiishi mwanamke huyo pamoja na hospitali aliyokuwa akifanyiwa matibabu.
Wakati huo huo, maafisa wakuu wa afya nchini Liberia pia walifanya mkutano siku ya Ijumaa ili kujadili suala la kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Ebola kufuatia kesi hiyo mpya iliyogundulika.
WHO iliwahi kutangaza kuangamizwa kwa Ebola tarehe 5 Mei 2015 na baadaye kesi mpya ikagundulika Novemba 2015 na kumalizika Januari 2016.
Source:trt.

0 MAONI YAKO:
Post a Comment