Rais Magufuli leo amekutana na Viongozi wa CCM ngazi za Mikoa na Wilaya kwa lengo la kuwashukuru kwa kazi nzuri walizofanya wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Katika hafla hiyo, Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa kwake na baadhi ya watu wanaowaonea huruma mafisadi ambao wamekuwa wakitumbuliwa hadharani
Amesema fisadi hastahili huruma kwa sababu yeye wakati anawaibia wananchi hakuwa na huruma
"Wapo Wanaodai Tunakiuka haki za Binadamu Kuwatangaza Wanaotumbuliwa.....Wao walikuwa Wanafanya sawa Kuwaibia Hadharani Watanzania? " Amehoji Rais Magufuli
Zaidi, msikilize kwenye video hii akiongea
0 MAONI YAKO:
Post a Comment