Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) mkoa wa Morogoro imeanzisha opersheni maalumu ya kuwachunguza watumishi wa umma,viongozi wa siasa,wakulima pamoja na wafugaji wanaojihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa hali inayosababisha migogoro ya ardhi kuendelea kushika kasi katika mkoa huo.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa Takukuru mkoa wa
Morogoro Emmanuel Kiyabo amesema taasisi hiyo imeokoa zaidi ya shilingi
milioni 27 fedha za miradi ya maendeleo zilizokuwa mikononi mwa
watuhumiwa zikiwemo fedha za mradi wa kuweka alama za barabarani
manispaa ya Morogoro ambapo amewataka viongozi wa vijiji kuacha maramoja
tamaa ya kupokea fedha za wafugaji kuwapatia maeneo ya malisho.
Kufuatia kukithiri kwa matukio ya viongozi wa serikali pamoja na
baadhi ya wabunge kukumbwa na kashfa za rushwa wakazi wa mji wa Morogoro
wameeleza kitendo hicho kimeondoa imani kwa wananchi kuwaamini wabunge
wao na wameziomba mamlaka husika kuwashugulikia kikamilifu wabunge
wanaokumbwa na kashfa hizo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment