April 03, 2016

Kikosi cha Geita Gold Mine
Kikosi cha Geita Gold Mine





KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa hukumu ya timu za daraja la kwanza zilizokuwa zinatuhumiwa kupanga matokeo katika michezo yao ya mwisho ya Kundi C, 

Hukumu hiyo ya Kamati ya Nidhamu iliyokutana jana, imeamua kuzishusha daraja timu za Geita Gold Mine, JKT Oljoro, Polisi Tabora na Kanembwa JKT, viongozi wa timu hizo na Refa na Kamisaa wa mchezo Kanembwa na Geita wamefungiwa maisha kujihusisha na mpira, huku wachezaji wakifungiwa miaka 10.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jamal Malinzi, Rais wa TFF, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, amesema: “Tuhuma za upangaji matokeo ligi daraja la kwanza klabu zote nne zimeshushwa daraja na viongozi wamefungiwa maisha.”
Malinzi pia aliendelea kusema kuwa wachezaji wamefungiwa miaka 10 kujihusisha na mpira wa miguu, kwa mujibu wa kanuni za kamati ya nidhamu zinavyofafanua.
Habari ambazo hazijathibitishwa zinasema kuwa sasa timu ya Mbao ya Mwanza ndiyo itakayoungana na Africans Lyon na Ruvu Shooting kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao.


Tuhuma za upangaji matokeo ligi daraja la kwanza vilabu vyote vinne vimeshushwa daraja na viongozi wamefungiwa maisha.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE