Kijana Hald Bitebo akiwa chini huku akiwa tayari ameshakata
Bitedo amekufa huku akiwa na moja ya vyuma hivyo chakavu mkononi
Polisi wamewasili eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu.
Askali Polisi akikagua vyumamaarufu sklepa alivyookota marehemu
Na Dustan Shekidele.
MOROGORO: Janga la Kitaifa! Wakati wasanii wa Bongo
Fleva, Rehema Chalamila "Ray C na Rashidi Makwilo "Chid Benz"
wakiteswa na madawa ya kulevya "unga" jamaa aliyefahamika kwa jina la
Halid Bitebo, mkazi wa Kaloleni Kata ya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro, anadaiwa
kuzidisha " dozi ya unga" kisha kuanguka na kufa katika Mtaa wa Kingo jirani na Faya.
Akizungumza na Mtandao huu, mmoja wa mashuhuda wa
tukio hilo lililojili maeneo hayo wikiendi iliyopita, Walidi Mkami alisema:
" Ilikuwa saa 12:00 asubuhi, vijana wawili wapita njia walitugongea
na kutujulisha kuwa nje ya nyumba yetu
kuna kijana (teja) amezidisha dozi ya madawa kisha ameanguka.
"kweli tulipotoka tulimshuhudia akiwa
ameshakata roho ndipo tukatoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa
wetu Mwajuma Ndege."
Kwa upande wake mwenyekiti huyo, alikiri kutokea
kwa tukio na kwamba ndiye aliyetoa taarifa polisi. Kabla ya polisi kufika eneo
la tukio, mwanahabari wetu alizungumza na kijana Waziri Rashid ambaye alidai
kumfahamu vyema jamaa huyo.
"Huyu ni teja na shughuli zake ni kuokota vyuma
chakavu. Kila siku tulikuwa tunamkanya aache kubwia unga, umeona sasa ameanguka
na kufa huku udenda ukimtiririka, kwa vyovyote alikuwa amezidisha dozi, alisema
Rashid.
Source:shekidele
0 MAONI YAKO:
Post a Comment