Mahakama
Kuu ya kanda ya Dodoma inayoendelea na vikao vyake mjini hapa,
imemhukumu mkazi wa kijiji cha Makanda Mpendoo Wilayani Manyoni Mkoa wa
Singida, Adriani Francis Januari (25), adhabu ya kunyongwa hadi kufa.
Adrian
amehukumiwa adhabu hiyo baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kumuawa
mfanyabiashara wa zao la ufuta mkazi wa Nzuguni Dodoma mjini, Enock
Kasimba nakisha kumnyang’anya shilingi 450,000/=.
Aidha,
mahakama hiyo iliwaachilia huru washitakiwa wengine katika kesi hiyo
namba 52/2014, Rehema Alli (25) mkazi wa Mbagala Dar -es -salaam na
Aidani Trancis (14) mkazi wa kijiji cha Makanda Mpendoo wilayani
Manyoni.
Washitakiwa hao waliachiliwa huru baada ya kukosekana kwa ushahidi wa kutosha kuwaunganisha na mauaji hayo.
Kaka
yake na mshitakiwa Adriani, ambaye anatuhumiwa kushiriki katika mauaji
hayo Raymond Francis, aliweza kutoroka na kukimbilia kusiko julikana.
Awali
mwendesha mashitaka mwanasheria wa serikali Petrida Muta, alidai mbele
ya jaji Hamisi Hamisi Kalombola kuwa mnamo mei 27 mwaka 2013 muda
usiojulikana, mshitakiwa na ndugu zake wengine watatu, kwa makusudi
walimuuwa Enock Kasimba kwa lengo la kumpora Shilingi 450,000.
Muta alisema siku ya tukio Adriani na wenzake walimtuma Aidan kumuita mfanyabiashara Enock kwa madai wanaufuta wa kumuuzia.
Alisema
Enock alipofika nyumbani kwa washitakiwa, alikamatwa kwa nguvu na kisha
kukabwa koo kwa lengo la kumzuia asipate pumzi, kitendo
kilichosababisha kufariki dunia papo hapo.
Mwanasheria
Muta, alisema baada ya mfanyabiashara Enock kufariki dunia,washitakiwa
hao walibeba mwili wake na kuupeleka hadi mto Bubu wa kijiji hicho cha
Makanda Mpendoo.
Akifafanua,
alisema washitakiwa Rehema na hasa Aidan ambaye ni mdogo wake na
Adriani, ushahidi wao umesaidia kwa kiasi kikubwa Jamhuri kumtia
hatiani mshitakiwa wa kwanza Adriani.
“Aidan
ameieleza mahakama jinsi alivyoitumwa na kaka zake kumwita
mfanyabiashara Enock na pia alisaidia kuwaonywesha askari polisi kaburi
alikozikwa Enock. Mwili wa Enock ulikaa kaburini kwa siku tano ndipo
ukafukuliwa kwa ajili ya daktari kuufanyia uchuguzi,” alisema Muta.
Kabla
ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mwendesha mashitaka Muta, aliiomba
Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa, ili iwe fundisho kwa
watu wengine wanaotarajia kuuwa binadamu wenzao kwa kukusudia.
Kwa
upande wake wakili wa kujitegemea kutoka Dodoma, Simioni Mwigulu
aliyekuwa anamtetea Adriani, alisema wanaiachia mahakama kuu, ifanye
maamuzi yake.
Akitoa
hukumu hiyo, Jaji Hamisa alisema ushahidi uliotolewa na upande wa
Jamhuri umethibitisha bila kuacha chebe chembe yo yote ya shaka na
hivyo,mshitakiwa ana hatia ya kosa aliloshitakiwa nalo.
Chanzo:dewjiblog
0 MAONI YAKO:
Post a Comment