May 04, 2016

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fisoo
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fisoo




Katika hatua za kupamba na kazi za filamu ambazo zinaingizwa nchini kinyume na sheria na kuikosesha serikali mapato, Bodi ya Filamu tayari imekamata zaidi ya kazi za filamu 656,000 ambazo zimeingizwa nchini kinyume na sheria.
Akizungumza na Bongo5 Jumatano hii, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fisoo alisema wao kama bodi ya filamu bado wanapambana na watu hao ambao wanaikosesha serikali mapato.
“Mpaka sasa hivi tumekamata kazi 656,000 na bado msako unaendelea,” alisema Joyce. “Sisi tunafanya huo msako lakini pia Wananchi wanatakiwa kutoa taarifa za watu kama wao ili kurahisisha namna ya kuwakamata,”
Katika hatua nyingine Joyce amewataka wasanii kupeleka kazi zao bodi ya filamu ili zikaguliwe kabla hazijaingia sokoni kuepuka kuingiza sokoni kazi ambazo hazina tija kwa Watanzania.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE