May 03, 2016


Madee2


                       

Msanii wa muziki kutoka Tip Top Connection, Madee amefunguka na kudai kuwa siku zote atamlaumu msanii wa Bongo flava na aliyewahi kuwa chini ya usimamizi wa Tip Top, Mb Doggy kwa kuondoka kwenye lebo hiyo.
Akizungumza katika kipindi cha Hatua Tatu cha Times Fm, Madee amedai Mb Dog alikosea kuondoka Tip Top kwa kuwa alikuwa chini ya mikono sahihi.
“Mimi kitu ambacho nitaendelea kumlaumu Mb Doggy ni kuondoka Tip Top, unajua unapokuwa kwenye malezi ya baba na mama mmoja hata maadili ni yale yale, unapoenda sehemu nyingine unakutana na vitu vipya, alafu si tulikuwa tukitoa nyimbo Babu tale ndiyo anaenda kushughulika kila kitu kupeleka Radio na vitu vingine, sasa hakuwa na menejimenti kila kitu alikuwa akifanya yeye baada ya kutoka nahisi ndiyo maana akashindwa” Alisema.
Kwa sasa MB Dog yupo chini ya label ya QS Mhonda Entertainment pamoja na Q Chief. Ambapo mpaka sasa ameshaachia kazi kadhaa, moja wapo ni video ya wimbo ‘Sio Siri’ ambayo ulifanya vizuri.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE