May 19, 2016

1

Mmoja kati ya wasichana 219 wanaoshikiliwa na kundi la Boko Haram nchini Nigeria ameokolewa akiwa na mtoto wa miezi 4.


2 
Amina Ali Nkeki akiwa na mwanae.
Amina Ali Nkeki (19) alipatikana akiwa amembeba mtoto huyo wa miezi minne na Jeshi lililokua likifanya doria siku ya Jumanne katika msitu wa Sambisa, jirani na mpaka na Cameroon
Msichana huyo alikutwa na mwanajeshi anayesadikiwa kuwa na mfuasi wa kundi la Boko Haram.
Kuokolewa kwake kumefanya wasichana 218 kutofahamika walipo baada ya kutekwa na kundi la Boko Haram Aprili 2014 katika shule ya sekondari Kaskazini- Mashariki mwa Nigeria.

3 
Mwananchi akiwa na bango linalotaka kuachiliwa kwa wasichana waliotekwa na Boko Haram.
Mwanajeshi huyo anayehisiwa kuwa ni wa kundi la Boko Haram amefahamika kwa jina la Mohammed Hayatu alikiri kuwa yeye ni mume wa Amina.
Mwanajeshi huyo amepelekwa kati mji wa Maiduguri pamoja na Amina na mwanae kwa ajili ya uchunguzi wa afya.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE