May 19, 2016

29
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imetoa ramani sahihi ya Tanzania inayoonyesha maeneo na mipaka kwa usahihi. Hatua hii imekuja baada ya Wizara hiyo kubaini matumizi ya ramani zisizo rasmi ambazo zinapotosha mipaka ya nchi.
Akizungumza wakati anaonyesha ramani hiyo Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya alisema kuwa wameamua kutoa ramani sahihi ili kuondoa upotoshaji uliopo mitaani.
Suala kubwa linalopotoshwa ni Ziwa Nyasa ambapo kwenye ramani za mitaani linaonekana lote lipo Malawi kitu ambacho sio sahihi hata kidogo.

1 
Ramani sahihi ya Tanzania.
Aidha alisema kuwa kutumia ramania ambayo isiyo sahihi kwa kujua au kutokujua ni kosa kisheria. Amewataka walimu na wote walioko katika nafasi ya kuelimisha jamii kutumia ramani hii.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE