May 19, 2016

Shirika la ndege la Misri (Egypt Air) limetoa taarifa za kupotea katika rada ndege ya shirika hilo iliyokua ikitokea Paris, Ufaransa ikielekea Cairo, Misri.

_89735812_franceegypt4640516
7 

Eneo ndege ilipopotelea.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa abiria 56, wahudumu wa ndege 7, na wanausalama 3 wamo katika ndege hiyo MS804.
Ndege hiyo aina ya Airbus A320 ilikuwa ikiruka umbali wa futi 37,000 (mita 11,300) ilipotelea ukanda wa Mashariki mwa Mediterranean. Maafisa walisema kuwa ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na rada saa 2:45 (00:45GMT) kwa saa za Cairo.
5 
Ndege aina ya Airbus A320 iliyopotea.

Taarifa zinaeleza kuwa ndege hiyo iliondoka katika mji wa Paris 23:09 muda wa huko siku ya Jumatano na ilitarajiwa kufika Mji Mkuu wa Misri 03:00 muda wa huko siku ya Alhamisi.
Harakati za kuitafuta na kuikoa ndege hiyo zinaendelea ili kuhakikisha watu wote wanakuwa salama.

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE