May 04, 2016

Jani

Mvulana wa umri wa miaka 10 nchini Finland ameshangaza wengi baada ya kugundua udhaifu katika mtandao wa kijamii wa Instagram.
Mvulana huyo kwa jina Jani ametunukiwa $10,000 (£7,000) baada ya kugundua udhaifu huo uliowezesha mtu kuingia kwenye mtandao huo wa kusambaza picha na kufuta maoni ya watu.
Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba kisheria haruhusiwi kutumia mtandao huo hadi atimize umri wa miaka 13.
Facebook, inayomiliki Instagram, ilichukua hatua upesi na kuondoa udhaifu huo.
Sasa, ndiye mtu mchanga zaidi kutunukiwa pesa kwa kugundua udhaifu katika mitandao ya kampuni hiyo.
Aliandikia wasimamizi wa mtandao huo barua pepe Februari kuwafahamisha kuhusu ugunduzi wake.
Wataalamu wa mtandao huo walimfungulia akaunti ndipo aweze kuthibitisha madai yake na akafanikiwa.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE