May 26, 2016

7
Wakati mashabiki wa muziki wa Tanzania wakiwa na matumaini makubwa kadiri siku zinavyozidi kwenda kuwa msanii wa muziki wa Hip Hop Rashid Mkwilo maarufu Chid Benz atarudia kwenye hali yake ya kawaida baada ya kuathirika na madawa ya kulevya, kumbe hali si kama wengi wanavyotarajiwa kwani inasemekana Chid Benz alishatoroka.
Msanii huyo alipelekwa katika nyumba ya matibabu ya waathirika wa dawa ya kulevya (Sober House) ili aweze kupatiwa matibabu baada ya kuathirika na utumiaji dawa za kulevya. Matokeo ya siku 28 za kwanza yalionyesha matumaini kuwa anaendelea vizuri. Lakini sasa Chid Benz hayupo tena kituoni hapo.
Mkuu wa kituo hicho akizungumza alisema kuwa ni kweli kuwa Chid Benz hayupo tena kwenye kituo hicho. Amesema kuwa alitakiwa kukaa kwa miezi 3 ili awe sawa lakini amekaa siku 28 tu. Aidha amesema kuwa siyo kwamba alikua akiishi vibaya, labda kwa vile hakuwa amezoea maisha ya kubanwa.
Aidha amesema kuwa kuna wakati Babu Tale alipokuja kumtembelea aling’ang’ania kuondoka naye lakini walimshauri abaki akakubali lakini baada ya muda hakuonekana tena.
Babu Tale hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo kama anafahamu chochote kuhusu kutoroka kwa Chid Benz katika nyumba ya matibabu na kusema muda muafaka ukifika atasema yote.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE