Hivi unajua kama Ali Kiba aliwahi kuwasimamia wasanii kadhaa chini ya
‘label’ yake kama tunavyoona kwa baadhi ya wasanii wa hapa nchini kwa
sasa,iliishia wapi ana mpango wa kurudi tena kusimamia wasanii.
‘’Hivi vitu nilikuwa navyo muda mrefu ila havikuwa
‘promoted’unajua vitu vyangu vingi huwa vinakuwa kimyakimya nilikuwa na
wasanii wengi lakini nilivyopumzika kufanya muziki kipindi kile ilibidi
niwapumzishe kwasababu ya vitu ambavyo vilitokea nilichukua likizo, na
sasa ili niweze kukaa sawa ndio lazima waweze nao kufanikiwa katika vitu
vyao vya muziki, siwezi mimi nikawa nimepumzika halafu mashabiki wakawa
wamenimis halafu nikamtoa msanii na watu wanielewa, hapana kiukweli
lazima niwe vizuri na nikawaonyesha msanii wangu si unaona hadi sasa
hivi nimerudi lakini mdogo wangu Abdul Kiba bado sijamleta lakini wapo
wasanii wengi kama Dalila, na wengine ambao hawajasikika lakini kazi zao
zipo studio, lakini kwasasa nipo vizuri ataanza Abdul na wengine
watafuata’’ Alisema Ali Kiba.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment