Muongozaji wa video za Bongo ambaye anafanya vizuri Msafiri Shabani kutoka kampuni ya Kwetu Studio amesema changamoto kubwa wanayokutana nayo waongozaji wa hapa nchini ni location.
Akiongea na E-Newz ya EATV, Msafiri alisema ameanza kwenda kufanya
video zake Afrika Kusini kutokana na uhakika na uharaka wa upatikanaji
wa vitu kwaajili ya kazi zao kwakuwa kwa Tanzania inachukua muda mrefu
wa kupata ruhusa ya kukamilisha kazi zao.

Pia Msafiri aliongezea kuwa sababu nyingine inayowafanya wakashuti video hizo nje ni kutokana na kuangalia wengine wanafanya nini ili nao waweze kushika nafasi nzuri katika soko la ushindani pia akidai kuwa inasaidia kupandisha thamani ya msanii kwakuwa anaonekana ana uwezo wa kutengeneza pesa kwaajili ya kufanya kazi zake.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment