June 18, 2016

Ni masaa machache yamepita toka taarifa zinazoripotiwa kutoka kwa shirikisho la soka barani Afrika CAF, kuripotiwa kuionya Yanga kutomtumia mchezaji Hassan Kessy hadi amalizane na Simba au Simba watoe barua ya kuridhia kumalizana na nyota huyo aliyejiunga na Yanga lakini mkataba wake unaisha mwezi June 31.
Ufafanuzi uliotolewa na CAF kupitia kwa afisa habari wake Junior Binyam ni kuwa Yanga wanaruhusiwa kumtumia mchezaji Hassan Kessy katika mchezo wa nane bora wa leo June 19 dhidi ya MO Bejaia ya Algeria ila kama watakuwa wamekamilisha taratibu zote za usajili wa CAF, kama ambavyo inatakiwa.
JUNIOR BINYAM-1
Junior Binyam
“Kama hakuna malalamiko kutoka katika klabu anayotoka ni jambo muhimu sana, baada ya hapo ni kuangalia usajili wa CAF kama umefanyika kwa usahihi kama kwenye mtandao au kawaida, ila suala la kuangalia kama mchezaji amemalizana na klabu yake ni muhimu”
“Ninaamini wachezaji wao watakuwa hawana tatizo kwa maana ya usajili wa CAF. Kwenye suala la usajili katika klabu walizotoka, hili tunaweza kusubiri chama cha nchi yenu (TFF) ndio waseme. Lakini hadi sasa, inaonekana wachezaji hao wanaweza kutumika, hilo tuwaachie wao (Yanga).”
CHANZO: Salehjembe

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE