Mshindi wa tuzo ya BET kwenye kipengele cha Best
International Act: Africa, Black Coffee amekamilisha kufanya collabo
yake na Alicia Keys.
Akiongea na Sunday Times, Black Coffee amekubali taarifa hizo kuwa za
kweli lakini alikataa kuweka kila kitu wazi kwa kusema, “can’t keep
telling people everything I’m doing, as it may bore people.”
Jina la Black Coffee limeonekana kuwa geni kwenye masikio ya wengi
lakini huyu ni mmoja kati ya wasanii wenye heshima kubwa Afrika Kusini
na mpaka sasa amefanikiwa kuachia albamu sita na tayari ameshakutana na
mastaa wakubwa akiwemo Diddy na Wiz Khalifa alipohudhuria tamasha la
Ultra Music [Festival] lililofanyika, March 2016, Miami.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment