
Maombi ya Kiislamu ya kuswaliwa kwa
jeneza la marehemu bondia mashuhuri duniani Mohammed Ali yamefanyika
katika jimbo la Kentucky, Marekani.
Ali alifariki wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 74.
Maelfu
ya watu, wakiwemo Waislamu kutoka maeneo mengi duniani, wamehudhuria
swala hiyo katika ukumbi wa Freedom Hall, mjini Louisville.

Maelfu ya watu wamehudhulia swala hiyo
Swala hiyo inapeperushwa moja kwa moja kupitia runinga na Waislamu
wengi duniani wanatumai kwamba itaashiria mchango mzuri kwa dini ya
Kiislamu nchini Marekani.
Muhammad Ali alisilimu
akiwa kijana. Alikuwa kwanza mwanachama wa madhehebu ya Nation of
Islam, kundi lililotetea haki za watu weusi, lakini baadaye akakumbatia
imani ya kawaida ya Kiislamu.

Muhammad Ali alifariki Ijumaa akitibiwa Arizona
Mazishi yake yatafanyika Ijumaa.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment