
Takriban maafisa 302 wa polisi
wamefutwa kazi nchini Kenya kwa kukataa kukaguliwa tangu mpango huo wa
kutaka kukabiliana na ufisadi kuanzishwa mwaka 2013,kulingana na tume
inayotekeleza ukaguzi huo.
Hayo yalibainishwa na Jonhston Kavuludi
,anayeongoza tume hiyo ya huduma za maafisa wa polisi huku maafisa wa
polisi wakijiandaa kuhojiwa na jopo katika mji wa magharibi wa Kisumu.
Ukaguzi
huo ni mpango wa uma na hufanywa mbele ya kamera ambapo maafisa uhojiwa
kuhusu mali na fedha wanazomiliki huku mgongano wowote wa maslahi
ukichunguzwa.
Mwezi uliopita wakati jopo hilo lilipokuwa Mombasa
,afisa mmoja wa idara ya trafiki hakuweza kusema ni wapi alipata
takriban dola 500,000 ambazo ziliwekwa katika mtandao wa simu unaotuma
fedha ama kupokea na akaunti yake ya benki.
Wakenya katika
mitandao ya kijamii walishangazwa na kuelezea vile wanavyolazimishwa
kutoa hongo baada ya kukamatwa kwa makosa ya trafiki.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment