June 09, 2016

13277779_909000139226068_175520434_n
Kwa mujibu wa Rich Mavoko, Diamond ni msanii mwenye moyo wa pekee.

Mavoko anadai kuwa bosi wake huyo hupigia debe kazi za wasanii wa label yake kuliko hata zake mwenyewe.
“Sisi huwa tunapanga strategy nzuri kabisa ya promotion kabla ya kutoa nyimbo akiwemo Diamond mwenyewe anakuwa mstari wa mbele sana kwa sisi. Mpaka sometimes mameneja wanamuambia ‘mbona wewe unakuwa mstari wa mbele sana kwenye kazi za wenzako.’ Lakini nafikiri ni moyo wa kujitolea kwamba anaamini alipofika mtu yoyote anaweza akafika kama akijituma,” Mavoko ameiambia Bongo5.
Kwa upande mwingine Mavoko amesema kufanya kazi chini ya label kuna tofauti kubwa sana.
“Kwa mfano mimi nilikuwa natoa nyimbo mara moja kwa mwaka, hiyo ilikuwa inawaumiza sana mashabiki wangu kwasababu wanafikiria ‘sasa Rich mbona anajua, mbona anatoa nyimbo kwa mwaka mara moja.’ Hiyo ilikuwa inawaumiza mpaka sometimes wanaandika kwenye Instagram, mimi sio kwamba sioni, naona lakini nitafanya nini, niko mwenyewe kila kitu nafanya mwenyewe, niwe meneja mimi, muimbaji mimi, nianze kupanga video mimi. Kwahiyo ninapokuwa na timu ambayo wana njaa na wanataka kufanya kazi yako ifike wewe upate na wao wapate utaona mabadiliko yako kwa haraka.”
Kuhusu kurekodi nyimbo Mavoko amesema kukesha kila siku WCB ni kawaida.
“Kama mimi nyimbo yangu tumekesha sana, nyimbo ya Raymond tumekesha sana, nyimbo za Harmonize tumekesha sana, Diamond ndio usiseme sababu katika wasanii ambao nimekutana nao katika maisha yangu ambao hawapendi kulala Diamond wa kwanza, simsifii kiukweli mimi sometimes mpaka ananiudhi ‘namuambia sasa Nasib ndugu yangu yaani mpaka sasa hivi saa moja asubuhi hatujalala,’, ‘wewe Rich tatizo lako unapenda sana kulala, utalala uzeeni, tutafute pesa.’ Kwahiyo unaona kabisa huyu mtu yupo namba moja lakini sijui anataka sasa kuwa zero, watu wana njaa kiukweli.”

                 

Related Posts:

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE