June 12, 2016

 
 Aliyekuwa Mwanachama wa CHADEMA, Bw.Goodluck Ole Medeye amehamia rasmi Chama cha UDP kinachoongozwa na Bw. John Cheyo na kukabidhiwa kadi ya uanachama leo. 

Ole Medeye ambaye pia aliwahi kuwa mbunge wa Arumeru Magharibi  Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi katika awamu ya nne, lakini pia aliteuliwa na vyama vinavyounda katiba ya wananchi UKAWA kuwania nafasi ya Uspika wa Bunge.

 
Medeye amezungumza kwa kujipambanua kuwa yeye anasimamia haki na demokrasia, na kwamba amekerwa sana na tabia ya vyama vya Upinzani kutomheshimu Naibu Spika,Dkt. Tulia Ackson Mwansasu,pichani kati ni Mwenyekiti wa chama cha UDP,Mh.John Cheyo akishuhudia tukio hilo.
Amezungumza hayo mbele ya mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho,Mwananyamala jijini Dar
 

Chanzo:ITV Tanzania

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE