June 12, 2016

Mfanya biashara maarufu nchini, Yussuf Mehboob Manji ataendelea kuiongoza Yanga kwa miaka mingine minne, baada ya kutetea nafasi yake katika uchaguzi uliofanyika jana ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Manji ambaye hakuwa na mpinzani, ameshinda kwa kukusanya zaidi ya asilimia 90 ya kura, huku Makamu wake, Clement Sanga akifanikiwa pia kutetea nafasi yake kwa kumshinda mpinzani pekee, Tito Osoro.
Sanga amekusanya zaidi ya asilimia 80 ya kura katika uchaguzi wa nafasi tatu, nyingine ikiwa ni Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro amesema  Manji ametangazwa mshindi baada  kupata kura 1, 468 kati ya 1,470 zilizopigwa huku kura mbili tu zikiharibika na hakukuwa na kura ya hapana,.
Muro amesema Sanga ameibuka mshindi  baada ya kujizolea kura 
1,428 kati ya 1,508 zilizopigwa, huku mpinzani wake wake pekee, Osoro akiambulia kura 80 tu.
 
Walioshinda nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji n:
Siza Augustino Lymo kura 1027, 
Omary Said Amir kura 1069, 
Tobias Lingalangala kura 889,
 Salum Mkemi kura 894, 
Ayoub Nyenzi kura 889, 
Samuel Lukumay kura 818, 
Hashim Abdallah kura 727 
Hussein Nyika kura 770.
 
Wajumbe wengine 12 waliogombea nafasi hiyo ni:
David Luhago kura 582, 
Godfrey Mheluka kura 430, 
Ramadhani Kampira kura 182, 
Edgar Chibura kura 72, 
Mchafu Chakoma kura 69, 
George Manyama kura 249, 
Bakari Malima kura 577, 
Lameck Nyambaya kura 655, 
Beda Tindwa kura 452,
 Athumani Kihamia kura 558, 
Pascal Lizer kura 178 
Silvester Haule kura 197.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE