June 26, 2016

Kipande kipya cha mabaki ya ndege kilichopatikana nchini Tanzania kitafanyiwa uchunguzi ili kubaini iwapo kinahusiana na mabaki ya ndege ya shirika la ndege la Malaysia MH 370 iliyopotea na kutofahamika ilikoelekea hadi hivi sasa.
Maelezo hayo ni kwa mujibu wa Shirika la Habari la Malaysia ambalo limemkariri waziri wa usafirishaji wa nchi hiyo, Liow Tiong Lai, akisema kuwa kipande hicho ni kikubwa na iwapo itathibitika kuwa ni cha ndege hiyo basi nchi hiyo itatuma wachunguzi nchini ili kuchunguza iwapo ni kweli kinahusiana na ndege ya MH 370 iliyopotea.
Aidha, Waziri Tiong Lai amesema mabaki ya ndege yaliyopatikana hivi karibuni katika ufukwe wa bahari ya Hindi huko nchini Madagascar na kufanyiwa uchunguzi hayakuwa na uhusiano wowote na ndege hiyo.

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE