UWANJA
wa Taifa, Dar es Salaam una uwezo wa kuchukua watu 60,000, lakini kesho
utafungwa wakati wa mchezo wa Yanga na TP Mazembe ya DRC baada ya
mashabiki 40,000 kuingia.
Hayo ni maagizo ya Kamisa wa mchezo huo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika, ambao mashabiki wataingia bure, Celestine Ntangungira kutoka Rwanda.
Na hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro alipozungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam.
Muro amesema kwamba mashabiki watakaobahatika kuingia uwanjani ni wale ambao watafika mapema na kwamba Yanga itatekeleza agizo la Kamisaa la kufunga mageti yote wakitimia watu 40,000.
Hayo ni maagizo ya Kamisa wa mchezo huo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika, ambao mashabiki wataingia bure, Celestine Ntangungira kutoka Rwanda.
Na hayo yamesemwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro alipozungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam.
Muro amesema kwamba mashabiki watakaobahatika kuingia uwanjani ni wale ambao watafika mapema na kwamba Yanga itatekeleza agizo la Kamisaa la kufunga mageti yote wakitimia watu 40,000.
Muro
amesema kwamba kutakuwa na ulinzi mkali wa askari Polisi kesho
kuhakikisha kwamba hazitokei vurugu za aina yoyote na watu wanaangalia
mchezo na kurejea nyumbani salama.
Wapinzani,
Mazembe waliwasili usiku wa jana na mshambuliaji Mtanzania, Thomas
Emmanuel Ulimwengu alipata mapokezi mazuri baada ya kutokeza nje ya
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
Mazembe
imekuja na kikosi cha wachezaji 18 ambao ni; Robert Kidiaba, Sylvain
Gbohou, Issama Mpeko, Joel Kimwaki, Thomas Ulimwengu, Christian Koume,
Jean Kasusula, Salif Coullbaly, Merveille Bope,
Jose
Badibake, Kissi Boateng, Roger Assale, Rainford Kalaba, Deo Kanda,
Adama Traore, Chriastian Luyindama, Nathan Sinkala na Joas Sakuwaha.
Maofisa wa benchi la Ufundi waliokuja ni Theobald Binamungu, Mohamed Kamwanya,
Dony Kabongo, Frederic Kitengie na Andre Ntime.
Madaktari
ni Hurbert Velud, Pamphile Mihayo, Mhudumu Richard Mubemb na Maofisa wa
Idara ya Habari na Mawasiliano, Heritier Yinduka, Arther Kikuni na
Meshack Kayembe.
Katika
mechi za kwanza za kundi hilo, Mazembe ilishinda 3-1 nyumbani dhidi ya
Medeama ya Ghana wakati Yanga ilifungwa 1-0 ugenini na MO Bejaia ya
Algeria Jumapili iliyopita.
Waamuzi
wa mchezo huo ni Janny Sikazwe wa Zambia atakayepuliza filimbi,
akisaidiwa na washika vibendera Jerson Emiliano Dos Santos wa Angola na
Berhe O'michael wa Eritrea.
Yanga
ilirejea nchini kwa awamu mbili Ijumaa na Jumamosi kutoka Antalya,
Uturuki ilipokuwa imeweka kambi kujiandaa na mchezo huo mara tu baada ya
mechi na MO Bejaia.
Kikosi kamili cha Yanga kilichokuwa kambini mjini ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’ na Benno Kakolanya.
Mabeki;
Hassan Kessy, Mwinyi Haji, Oscar Joshua, Andrew Vincent ‘Dante’, Mbuyu
Twite, Kevin Yondan, Pato Ngonyani, Vincent Bossou na Nahodha Nadir
Haroub 'Cannavaro'.
Viungo;
Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi, Said Juma ‘Makapu’, Simon Msuva, Haruna
Niyonzima, Deus Kaseke, Godfrey Mwashiuya na Obrey Chirwa.
Washambuliaji;
Donald Ngoma, Matheo Anthony na Amissi Tambwe, chini ya Kocha Mkuu,
Mholanzi, Hans van der Pluijm, Kocha Msaidizi Juma Mwambusi, Kocha wa
makipa, Juma Pondamali, Daktari Edward Bavu, Mchua Misuli, Jacob
Onyango, Mtunza Vifaa Mohammed Mpogolo na Meneja Hafidh Saleh.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment