June 25, 2016

gareth-bale-23324
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli akisalimiana na Viongozi mbalimbali muda mfupi uliopita wakati akienda kufungua Kituo cha Mawasiliano cha Jeshi la Polisi #callcenter kilichopo Central Polisi. #PolisiMpya

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. @mwigulunchemba, #IGP Ernest Mangu na wadau wengine wa maendeleo wa ndani na nje ya Tanzania. #PolisiMpya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amelitaka jeshi la polisi kutenda kazi zake ipasavyo ili ahadi walizoahidi wananchi wakati wa kampeni ziweze kutekelezeka na kusahau dosari zote zilizowahi kujitokeza kwenye jeshi la polisi.

Rais Magufuli amesema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kituo cha Mawasiliano cha Polisi ambacho kitarahisisha mawasiliano kwa upatikanaji wa taarifa za wahalifu kutoka kwa wananchi.
“Polisi ukimuona jambazi ana silaha kwanini usimnyang’anye haraka haraka kwa sababu uwezo na mafunzo mnayo. Ingawa kwenye upolisi kuna dosari ila tusahau yaliyopita na tungange yaliopo na yajayo,” alisema.
Aidha aliwataka polisi wasimamie kwenye kutenda mambo mazuri ili na wao kama wanasiasa waweze kutekeleza kile walichowaahidi wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu.
Aliendelea kwa kusema, “Nawaomba sana mniache nimalize niliyoyaahidi niyatimize kwa kipindi hiki cha miaka mitano sitegemei mtu aje kunichelewesha,” alisema Dkt Magufuli.”

0 MAONI YAKO:

Post a Comment

Popular Posts

WADAU

BLOG ZINGINE