
Shirikisho la soka Ulimwenguni
(FIFA) limetoa Ratiba ya Kombe la Dunia kwa Klabu ambalo litadhaminiwa
na Alibaba E-Auto na kufanyika huko Japan kati ya Desemba 8 na
18.Mashindano haya yatashindaniwa na Klabu 6 Mabingwa wa Mabara pamoja
na Mwakilishi kutoka Nchi Mwenyeji Japan.
Mechi za Mashindano haya
zitachezwa huko Suita City Football Stadium Mjini Osaka na
International Stadium Yokohama, Mjini Yokohama ambako pia ndipo
itachezwa Fainali .Hadi sasa Klabu 3 zimeshathibitika kucheza michuano hiyo ambazo ni Real Madrid, Mabingwa wa Ulaya, waliotwaa Ubingwa wao Mwezi Mei, na Timu nyingine ni Club America ya Mexico na Auckland City FC ya Mexico Bara la Oceanic ambazo zilitwaa Ubingwa wao Mwezi Aprili.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment