Waziri
Mkuu wa Uingereza, David Cameron amesema kuwa Theresa May atakuwa
waziri mkuu wa nchini hiyo baada ya yeye kuachia madaraka jumatano
jioni.
Theresa May ambaye alikuwa akipigia
chapuo nchi hiyo kutojiondoa ndani ya Muungano wa Ulaya atairithi mikoba
ya Cameron baada ya yeye kutangaza kuwa ataachia wadhifa huo kufuatia
nchi hiyo kupiga kura ya kujitoa katika Muungano wa Ulaya.
May amebakia yeye kutwaa nafasi hiyo
baada ya mwanasiasa Andrea Leadsom kujiweka pembeni kwa madai kuwa
Uingereza inataka kiongozi imara na anaamini kuwa May anaweza kazi hiyo.

Waziri Cameron atahudhuria mkutano
wa mwisho wa baraza siku ya Jumanne na atajibu maswali siku ya Jumatano
asubuhi na jioni atakabidhi barua yake ya kujiuzulu kwa Malkia.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment