
Maafisa wawili wa timu ya Atlabara
ya Sudan Kusini wameuawa katika machafuko yaliyotikisa mji mkuu wa Juba
kuanzia Alhamisi juma lililopita.
Shirikisho la soka la Sudan
Kusini limetangaza kuwa maafisa 2 wakuu wa mabingwa hao watetezi wa
ligi kuu ya Sudan Kusini walipigwa risasi na watu wasiojulikana
''Bwana William Batista na Leko Nelson walipigwa risasi usiku wa kuamkia jumamosi.'' alisema mkuu wa wa SFA bwana Chabur Goc.

''Tunaomba mwenyezi mungu awaweke mahali pema peponi'' alisema bw Goc.
Mapigano yamekuwa yakiendelea kwa siku kadha kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais Salva Kiir na wanajeshi watiifu kwa makamu wa Rais Dkt Riek Machar.

Vituo vya Umoja wa Mataifa pamoja na maeneo ya raia pia yameshambuliwa, jambo ambalo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linasema huenda likawa uhalifu wa kivita.
Takriban watu 200 wengi wao wakiwa wanajeshi wameuawa katika machafuko hayo.
0 MAONI YAKO:
Post a Comment